Mtindo wa Maisha, Mafunzo, na Uzidishaji wa M28 (M28 Plan)

Written on 05/01/2024
Gordon Decker

Mafunzo ya M28 - Utangulizi

Mafunzo ya Kimataifa ya Uanafunzi ya M28
Mafunzo haya yameandaliwa kwa ajili ya wale wanaokusudia kuwafikia wanafunzi wa Kimataifa  (au wengine wanaomtafuta Mungu) kwa upendo na ujumbe wa Yesu Kristo, kuwaongoza kumwamini Kristo, na kuwawezesha wawe wanaowafanya wengine pia kuwa wanafunzi katika tamaduni zao (au kokote ambako Mungu atawapeleka).

Programu Tumishi hii ina taarifa zote zinazohitajika kwa ajili ya kutekeleza Mafunzo ya Kuanzisha M28 kwa muda upatao saa nane (mfano Ijumaa jioni na Jumamosi asubuhi na mchana, au Jumamosi asubuhi na mchana, au ratiba nyingine zinazowezekana).
 
Maono yetu ni kuona mataifa yakibadilishwa kwa kuzidishwa kwa idadi ya jamii zinazowafanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu katika kila ngazi ya jamii – kwa kutumia Mpango wa Kimataifa wa Uanafunzi wa M28. Tunakukaribisha wewe nawe kujiunga nasi katika fursa hii ya ajabu ya kuugusa ulimwengu!

Mada za kawaida za mafunzo ni pamoja na:

  • Hitaji, Maono, na Mkakati wa M28
  • Kanuni, Tunu, na Misingi ya Upekee wa M28
  • Nyenzo, Mchakato, na Vifungu vya Maandiko vya M28
  • Uzoefu wa Ugunduzi wa Biblia wa M28
  • Mpango wa Huduma Binafsi wa M28

Tafadhali wasiliana nasi ili kujua zaidi kuhusu fursa za Mafunzo za M28.