Mwongozo wa Kikundi (Group Guidelines)

Written on 05/02/2024
Gordon Decker

Maelekezo yafuatayo husaidia kulifanya kundi na mwezeshaji kujikita kwenye lengo na tunu za muda wa ugunduzi wa Biblia.
 
Mwongozo wa Kikundi

  • Kila mmoja atoe maelezo kwa sentensi moja, siyo kwa aya (kuepuka mtu yeyote kutawala mno mjadala).
  • Jikiteni kwenye mambo yanayotokana na kifungu tu (siyo vifungu vingine).
  • Jikiteni kwenye mambo ambayo kundi hili  linayazingatia (siyo mitazamo ya watu wengine au nje ya vyanzo).
  • Wape watu muda wa kuitikia (usiogope ukimya ila ruhusu watu “kupita” kama wanataka kufanya hivyo).

 Mwongozo wa Mwezeshaji

  • Wezesha, usifundishe (tumia Mwongozo wa Mwezeshaji).
  • Hakikisha kipindi kinaenda kwa muda uliopangwa – Maliza kila sehemu ya ratiba. (Jumuika 25%, Gundua 50%, na Itikia 25%)
  • Kwa maswali kuhusu kifungu: “Ni nini katika kifungu hiki kinatusaidia kujibu swali?" (Lengo ni kusaidia Kikundi kuona kwamba kila mmoja anaweza kuielewa Biblia.)
  • Kwa maswali ambayo HAYAKO kwenye kifungu: “Tafadhali tujadili hili kwa kina baada ya muda wa kikundi” au “Hebu tuandae somo mahsusi wakati mwingine kutokana na kifungu ambacho kinajibu swali hilo.”
  • Kuhusu tafsiri au majadiliano “ya ajabu ajabu” au “potofu”: “Hilo linapatikana kwenye kifungu hiki?” Uliza kikundi kama wanaona jambo hilo hilo (hujenga mazingira ya kujisahihisha wenyewe). Kumbuka, “Lengo la leo ni kujikita kwenye yale ambayo kifungu hiki kinasema.”

Baada ya kikundi kudumu kwa majuma mawili au matatu, usiruhusu watu wapya kujiunga. Ikiwa watu wanataka kuleta wengine baada ya muda huo, wasaidie kuunda kikundi kipya.