Mwongozo wa Mwezeshaji (Facilitator's Guide)

Written on 05/03/2024
Gordon Decker

Maeneo matatu muhimu ya kila kipindi cha Ugunduzi wa Biblia wa M28 ni: Jumuika, Gundua, na Itikia. Mwezeshaji huongoza Kikundi kupitia utaratibu ufuatao.

Jumuika

  • Je, una nini cha kukufanya ushukuru leo?
  • Je, Katika juma hili umemwona Mungu akitenda kazi kwa namna gani katika maisha yako?
  • Je, ni changamoto gani unakabiliana nazo katika maisha? Tunaweza kukusaidia vipi?
  • Je, somo la ugunduzi lililopita ulilitumiaje? Ni mambo gani yalitokea?
  • Je, ni akina nani uliwashirikisha kuhusu ugunduzi wa kipindi kilichopita? Waliitikiaje?

Gundua

Hatua ya 1: Washiriki wasome sehemu fungu la Maandiko kwa zamu (fafanua maneno mapya/msamiati)

Hatua ya 2: Mtu mmoja asome fungu zima kwa sauti wakati wengine wakisikiliza

Hatua ya 3: Mshiriki mmoja aelezee kifungu kinavyosema kwa maneno yake mwenyewe (wengine waongezee mawazo yao)

 

Uliza/Jibu:

  • Je, unaona nini katika fungu hili?
  • Je, kinamaanisha nini kwako?
  • Je, ni kitu gani kimekuvutia /Je ni kitu gani hujakipenda kuhusu fungu hili?
  • Je, ni kwa namna gani fungu hili limebadili namna unavyomwona Mungu/Watu?

Itikia: kama hii ni kweli…

  • Je, ni kwa namna gani Neno linaweza kubadili jinsi unavyoishi?
  • Je utamshirikisha nani kuhusu ugunduzi huu wa leo?

Hitimisho

  • Amueni ni lini kikundi kitakutana tena
  • Fungeni kwa maombi (kwa ajili ya mahitaji yaliyotajwa mwanzoni)