Vifungu vya Mtindo wa Maisha ya Uanafunzi (Disciple's Lifestyle)

Written on 05/06/2024
Gordon Decker

Ifuatayo ni orodha pendekezwa ya vifungu kwa ajili ya wale ambao wameamua kumfuata Yesu, na ambao wanatamani kukuza mtindo wa maisha ya utii kwa Bwana na Mfalme wao. Vifungu hivi vinaeleza baadhi ya kanuni muhimu na misingi ya mwenendo wa maisha ya Kikristo. Tafadhali fuata hatua zilizoonyeshwa hapo chini ili kugundua ukweli na kanuni za mtindo wa maisha zinazofundishwa katika kila kifungu.


Jumuika:

  • Je, una nini cha kukufanya ushukuru leo?
  • Je, katika juma hili umemwona Mungu akitenda kazi kwa namna gani katika maisha yako?
  • Je, ni changamoto gani unakabiliana nazo katika maisha? Tunaweza kukusaidia vipi?
  • Je, somo la ugunduzi lililopita ulilitumiaje? Ni mambo gani yalitokea?
  • Je, ni akina nani uliwashirikisha kuhusu ugunduzi wa kipindi kilichopita? Waliitikiaje?

Maelekezo:

Tafadhali tumia hatua zifuatazo kukuongoza katika ugunduzi wa kweli ya Mungu katika kifungu cha Maandiko hapo chini.

Je, ninahitaji  kupitia Mwongozo wa Kikundi?

Gundua

Hatua ya 1: Washiriki wasome sehemu fungu la Maandiko kwa zamu (fafanua maneno mapya/msamiati)

Hatua ya 2: Mtu mmoja asome fungu zima kwa sauti wakati wengine wakisikiliza

Hatua ya 3: Mshiriki mmoja aelezee kifungu kinavyosema kwa maneno yake mwenyewe (wengine waongezee mawazo yao)

Uliza/Jibu:

  • Je, unaona nini katika fungu hili?
  • Je, kinamaanisha nini kwako?
  • Je, ni kitu gani kimekuvutia /Je ni kitu gani hujakipenda kuhusu fungu hili?
  • Je, ni kwa namna gani fungu hili limebadili namna unavyomwona Mungu/Watu?

Itikia: kama hii ni kweli…

  • Je, ni kwa namna gani Neno linaweza kubadili jinsi unavyoishi?
  • Je utamshirikisha nani kuhusu ugunduzi huu wa leo?

Mtindo wa Maisha wa Wanafunzi – Vifungu vya Maandiko

Uwepo wa Mungu (Zaburi 34:1-10; Isaya 55:1-7)
Ibada (Zaburi 9, Zaburi 95:1-7, Mathayo 4:8-11)
Neno la Mungu (Yoshua 1:7-8, Zaburi 119:24-35, Zaburi 119:72-74, Zaburi 119:89-94)
Utii (Zaburi 119:1-8, Zaburi 128:1-4, Yohana 14:23-24)
Maombi (Luka 18:1-8, Mathayo 6:5-13, Waefeso 6:10-20)
Toba (1 Yohana 1:5-10, Yakobo 5:16)
Msamaha (Mathayo 18:21-35)
Ushirika (Matendo ya Mitume 2:41-47)
Huduma (Mathayo 20:25-28)
Ushuhudiaji (Mathayo 28:18-20, Matendo ya Mitume 1:6-8)


Je, bado hujajiunga na Kikundi?
​Tafadhali tumia fomu ya Mwitikio wa Ugunduzi wa Biblia wa M28 kama unapitishwa katika mpango huu peke yako.