20. Yesu Abatizwa
Jumuika:
- Je, una nini cha kukufanya ushukuru leo?
- Je, katika juma hili umemwona Mungu akitenda kazi kwa namna gani katika maisha yako?
- Je, ni changamoto gani unakabiliana nazo katika maisha? Tunaweza kukusaidia vipi?
- Je, somo la ugunduzi lililopita ulilitumiaje? Ni mambo gani yalitokea?
- Je, ni akina nani uliwashirikisha kuhusu ugunduzi wa kipindi kilichopita? Waliitikiaje?
Maelekezo:
Tafadhali tumia hatua zifuatazo kukuongoza katika ugunduzi wa kweli ya Mungu katika kifungu cha Maandiko hapo chini.
Je, ninahitaji kupitia Mwongozo wa Kikundi?
Gundua
Hatua ya 1: Washiriki wasome sehemu fungu la Maandiko kwa zamu (fafanua maneno mapya/msamiati)
Hatua ya 2: Mtu mmoja asome fungu zima kwa sauti wakati wengine wakisikiliza
Hatua ya 3: Mshiriki mmoja aelezee kifungu kinavyosema kwa maneno yake mwenyewe (wengine waongezee mawazo yao)
Yesu Abatizwa (Yohana 1:29-34)
29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. 32Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. 34Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.
[Swahili Union Version (SUV): © -1952, 1997: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.]
Uliza/Jibu:
- Je, unaona nini katika fungu hili?
- Je, inamaanisha nini kwako?
- Je, ni kitu gani kimekuvutia /Je ni kitu gani hujakipenda kuhusu fungu hili?
- Je, ni kwa namna gani fungu hili limebadili namna unavyomwona Mungu/Watu?
Itikia: kama hii ni kweli…
- Je, ni kwa namna gani Neno linaweza kubadili jinsi unavyoishi?
- Je utamshirikisha nani kuhusu ugunduzi huu wa leo?