13. Baraka za Msamaha
Jumuika:
- Je, una nini cha kukufanya ushukuru leo?
- Je, katika juma hili umemwona Mungu akitenda kazi kwa namna gani katika maisha yako?
- Je, ni changamoto gani unakabiliana nazo katika maisha? Tunaweza kukusaidia vipi?
- Je, somo la ugunduzi lililopita ulilitumiaje? Ni mambo gani yalitokea?
- Je, ni akina nani uliwashirikisha kuhusu ugunduzi wa kipindi kilichopita? Waliitikiaje?
Maelekezo:
Tafadhali tumia hatua zifuatazo kukuongoza katika ugunduzi wa kweli ya Mungu katika kifungu cha Maandiko hapo chini.
Je, ninahitaji kupitia Mwongozo wa Kikundi?
Gundua
Hatua ya 1: Washiriki wasome sehemu fungu la Maandiko kwa zamu (fafanua maneno mapya/msamiati)
Hatua ya 2: Mtu mmoja asome fungu zima kwa sauti wakati wengine wakisikiliza
Hatua ya 3: Mshiriki mmoja aelezee kifungu kinavyosema kwa maneno yake mwenyewe (wengine waongezee mawazo yao)
Baraka za Msamaha (Zaburi 32)
1 Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. 2 Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila. 3 Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa Kwa kuugua kwangu mchana kutwa. 4 Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi. 5 Nalikujulisha dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. 6 Kwa hiyo kila mtu mtauwa Akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye. 7 Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso, Utanizungusha nyimbo za wokovu. 8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama. 9 Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. Kwa matandiko ya lijamu na hatamu Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia. 10 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka. 11 Mfurahieni BWANA; Shangilieni, enyi wenye haki Pigeni vigelegele vya furaha; Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.
[Swahili Union Version (SUV): © -1952, 1997: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.]
Uliza/Jibu:
- Je, unaona nini katika fungu hili?
- Je, inamaanisha nini kwako?
- Je, ni kitu gani kimekuvutia /Je ni kitu gani hujakipenda kuhusu fungu hili?
- Je, ni kwa namna gani fungu hili limebadili namna unavyomwona Mungu/Watu?
Itikia: kama hii ni kweli…
- Je, ni kwa namna gani Neno linaweza kubadili jinsi unavyoishi?
- Je utamshirikisha nani kuhusu ugunduzi huu wa leo?