Mtindo wa Maisha wa M28 (Lifestyle)

Written on 05/10/2024
Gordon Decker


Mtindo wa Maisha wa M28

Kiini cha M28
Kwenye kiini cha M28 kuna maeneo matatu ya msingi:
Maombi ya Dhati, Neno la Mungu, na Roho Mtakatifu.

Maombi ya Dhati

Kanuni: Maombi ndiyo jukumu kuu
Kusudi: Kudumu katika hali ya kumtegemea Mungu
Maelezo: Kudumu katika hali ya kutegemea uongozi na kazi ya Roho Mtakatifu - kwa njia ya maombi yasiyokoma, yanayoleta matokeo ya kutegemea msaada wa Mungu, ulinzi, uwezo, na makusudi ya Mungu kufunuliwa na kutimizwa
Vifungu vya Biblia: Luka 6:12; Wafilipi 4:6-7; Waefeso 6:18-20
Vitendo: Ombea milango kufunguka (mioyo), hekima, ujasiri, kuguswa, na toba
 
Neno la Mungu
Kanuni: Neno la Mungu ni Ukweli wa milele utakaoweka wazi dhamira zetu, kupima imani zetu, kubadilisha mioyo yetu, na kuelekeza mienendo yetu.

Kusudi: Kuiamini Biblia kama chanzo chetu cha uhakika cha kweli na mwongozo wa maisha yetu.

Maelezo: Kuliendea Neno la Mungu (Biblia) nyakati zote kwa ajili ya kweli, hekima, miongozo, na faraja katika hali zote na maeneo katika mbalimbali ya maisha

Vifungu vya Biblia: Luka 21:33; 2 Timotheo 3:16; Waebrania 4:12; Yoshua 1:8

Vitendo:Washirikishe wengine jinsi Neno la Mungu linavyokuongoza, kukufundisha, kukurekebisha, na kukutia moyo wewe binafsi.

Roho Mtakatifu
Kanuni: Roho Mtakatifu ndiye Msaidizi na Kiongozi wetu wa kweli

Kusudi: Kutegemea uongozi wa Roho Mtakatifu

Maelezo: Kujifunza kumtegemea Roho Mtakatifu kama Mwalimu, Kiongozi, Msaidizi, na Mlinzi wetu

Vifungu vya Biblia: Yohana 14:26; Marko 13:11; Matendo ya Mitume 1:8; Matendo ya Mitume 2:38; Matendo ya Mitume 5:32

Vitendo: Uwe kielelezo katika kutegemea maombi.


Omba

Kanuni: Maombi ndiyo jukumu letu kuu

Kusudi: Dumu katika hali ya kumtegemea Mungu

Maelezo: Kudumu katika hali ya kutegemea uongozi na kazi ya Roho Mtakatifu-- kwa njia ya maombi yasiyokoma kwa ajili ya kupata msaada wa Mungu, ulinzi, nguvu, na kufanya makusudi ya Mungu kufunuliwa kutimizwa na kwetu.

Vifungu vya Biblia: Mathayo 21:21-22; Luka 18:1-8; Waefeso 6:18-20; Wafilipi 4:6; Yakobo 5:13-18

Vitendo: Omba kwa ajili ya …

Milango/mioyo kufunguka

Hekima

Ujasiri

Kuguswa

Toba


Bariki

Kanuni: Mbegu (Neno la Mungu) hujua kinachotakiwa kufanywa kwenye udongo wa mioyo ya watu

Kusudi: Kudhihirisha nguvu ya Injili inavyoweza kubadili maisha kwa kubariki kupitia vinywa na matendo yetu.

Maelezo: Kutoa nafasi kwa wanafunzi wanaotoka katika mataifa mengine kukutana na upendo wa Kristo kwa vitendo na kusikia shuhuda za uwezo wa Neno la Mungu linalobadilisha maisha

Vifungu vya Biblia: Luka 6:28; Warumi 12:21; Wagalatia 6:9; Yakobo 3:13; 1 Petro 3:9

Vitendo: 

Kidhi mahitaji (unapoweza).

Peleka mahitaji kwa Yesu (ambayo huna uwezo nayo).

Toa shuhuda za uwepo, msaada, na uwezo wa Mungu. 

Shuhudia Neno:

Neno la Mungu (jinsi Biblia inavyoongea na wewe)

Kazi ya Mungu (jinsi anavyobadilisha maisha yako)

Njia za Mungu (jinsi anavyokuongoza/kukupa mahitaji yako)


Tafuta

Kanuni: Fanya kazi mahali ambapo Mungu anajidhihirisha kwa kazi zake – tafuta watu walio na mahitaji ya kiroho (ambao tayari Mungu anafanya kazi ndani ya mioyo yao)

Kusudi: Kubaini na kuwashuhudia watu wenye mahitaji ya kiroho kwa njia ya mazungumzo ya kutafuta ukweli.

Maelezo: Kwa kufuata mfano wa Yesu Kristo, tunawabaini na kuwashuhudia wale tu walio na kiu ya dhati ya kiroho.

Vifungu vya Biblia: Luka 19:10; Luka 10:1-11, 16; Luka 15:11-32

Vitendo: Uliza maswali kuhusu…

  • Mambo wanayopendelea
  • Vitu vinavyowavutia (watu/matukio)
  • Matumaini/ndoto zao
  • Malengo/matamanio yao
  • Changamoto/mizigo yamambo yanayowasumbua
  • Makusudi/hatma yao
  • Kinachowavutia katika uvumbuzi wa hatma ya Mungu katika maisha yao.

Gundua

Kanuni: Ukweli wa Mungu hubadilisha maisha. Wasaidie wanaomtafuta Mungu kuugundua Ukweli wa Mungu katika Neno lake.

Kusudi: Wezesha watu kuigundua KWELI

Maelezo: Kuwapa watu wenye kiu ya ya kweli ya kiroho, pamoja na jamii zao, nafasi ya kuigundua kweli (Ukweli wa Mungu), na kuwafikishia ujumbe wa Yesu Kristo uletao uzima.

Vifungu vya Biblia: Mathayo 10:5-8; Waebrania 4:12; Matendo ya Mitume 6:7; Matendo ya Mitume 13:16-41

Vitendo: Elezea kuhusu kusudi la awali la Mungu, uasi wetu, Karama ya Mungu, na mwitikio wetu unaohitajika.


Fuata

Kanuni: Wanafunzi wa Yesu walio watiifu huzaa matunda. Jamii yenye kupenda haki na kweli huvutia. Wasaidie wenye njaa ya kiroho kumfuata Yesu na kukua kiroho katika jamii ya wafuasi wa Kristo.

Kusudi: Kuonesha kuwa uanafunzi wa Yesu ni mtindo wa maisha.

Maelezo: Kuweka mazingira na mahusiano ambayo wafuasi wapya watakuwa wanakutana kama jamii ya Kibiblia inayofuata mtindo wa maisha wa uanafunzi wa Yesu.

Vifungu vya Biblia: Yohana 17:18-23; Matendo ya Mitume 2:42-47; Mathayo 28:18-20; Marko 4:20; Yohana 15:8, 16

Vitendo: Weka msingi wa kugundua kweli, utii, ibada, maombi, ushirika, kujaliana/huduma, na ushuhuda/umisheni.


Zidisha

Kanuni: Wanafunzi watiifu huzaa matunda na kuwabadilisha wenzao na kuwa wanafunzi wa Yesu. Huwawezesha waamini wapya kuwa na uwezo wa kueneza mbegu ya Neno la Mungu kwa jamaa na marafiki zao.

Kusudi: Kuwaandaa na kuwatuma wanafunzi kuwa wanaowafanya wegine kuwa wanafunzi.

Maelezo: Kuwaandaa na kuwatuma wanafunzi watakaowatafuta wengine ambao wana kiu ya kiroho, kuwashuhudia (wao na jamii zao), na kuwaongoza katika kugundua ukweli, na kuwawezesha kuwa wanafunzi wanaowafanya wengine kuwa wanafunzi pia.

Vifungu vya Biblia: Mathayo 28:18-20; Marko 4:20; Marko 16:15; Yohana 15:8,16; 2 Wakorintho 5:17-20; 2 Timotheo 2:2

Vitendo: Tengeneza mfano wa mfumo wa maisha ya kuabudu, neno la Mungu, Utii, Maombi, Ushuhudiaji, Ushirika, na Huduma/Kujali, Fundisha kuhusu wito wao (kujitambua), umisheni (kusudi), maono (fursa), na malezi (ufuatiliaji)